Okoa Mazingira Yetu. Pika Kwa Haraka. Tumia Kuni Mbadala
Kuwa mdau wa Mazingira kwa kutumia kuni za kisasa. Usiwe tena sababau ya miti kukatwa. Ni rahisi kutunza miti kuliko kupanda miti. Tumia Kuni Smart zenye ubora na safi kwa mazingira. Zinafaa kwa matumizi ya Nyumbani, taasisi kama mashule na Viwandani.
+255 757 156 338
Tupigie Tukuhudumie!

Bei Nafuu
Utaokoa gharama hadi asilimia 30 kwa kutumia KuniSmart. Inafaa kwa matumizi ya taasisi kama mashule.
Rafiki kwa Mazingira
Hatukati miti. KuniSmart ni nishati mbadala inayotengenezwa kwa mabaki ya mimea mashambani.
Ufanisi Mkubwa
KuniSmart zinatoa joto la kutosha na ni rahisi kushika moto. Hutasumbuka tena kuwasha moto na kusubiri.
Hazina Moshi Mwingi
Tofauti na kuni za kawaida, KuniSmart hazitoi moshi mwingi, hivyo ni nzuri kwa Afya yako pia.
Fahamu Kuhusu Tabianchi
Kwanini Utumie Kuni na Mkaa Mabadala?
Kuokoa Miti na Usafi wa Mazingira
Mimea kama miti ni Uhai. Lakini uoto wa miti kwenye mazingira yetu unazidi kuisha kila dakika. Na ni gharama zaidi kupanda miti kuliko kutunza miti. Hivyo kuepuka miti mingine kuendelea kukatwa, wewe kama mdau wa mazingira unapaswa kutumia nishati mbadala kwa mahitaji yako ya kupika. Ndiyo maana tumekuletea KuniSmart. Kuni hizi tunazitengeneza kwa kukusanya taka zinazotokana na mabaki ya mimea mashambani, amabazo mara nyingi hutupwa kwenye majalala ya halmashauri na kuchomwa. Hivyo tunafanya mazingira kuwa safi pia.
Kuepuka Janga la Mabadiliko ya Tabianchi
Bila shaka umeshuhudia matatizo kama Ukame, Mazao kukauka shambani kutokana na mvua kutokunyesha; kitu kinachopelekea baa la njaa. Matatizo haya na mengine yanatokana na shughuli za binadamu kama vile kukata miti na kutumia nishati chafu inayoathiri tabianchi. Hivyo ili kuepuka majanga haya, unashauriwa kutumia nishati mbadala kama hii KuniSmart.

Wasiliana Nasi
Kwa Oda za Kuni Zetu Pamoja na Maswali Mengine.
Tunapatikana: Kisesa, Mwanza, Tanzania
Tupigie: +255 757 156 338
Email info@kunisafi.co.tz/chabrienergyltd@gmail.com